http://s.rfi.fr/media/display/7f226e0a-4f37-11ea-af4c-005056a964fe/w:1024/p:16x9/000_Par7857853_0.jpg
Kizito Mihigo mbele ya vyombo vya habari, mjini Kgali Aprili 15 mwaka 2014, siku moja baada ya tangazo la kukamatwa kwake kutolewa.AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI

Rwanda: Maswali yaibuka kuhusu kutoweka kwa mwimbaji wa injili Kizito Mihigo

by

Maswali mengi yameibka kuhusu hatima ya mwimbaji wa injili Kizito Mihigo, ambaye hajaonekana tangu Alhamisi asubuhi. Ndugu zake wanaamini kuwa anazuiliwa.

Mihigo aliachiliwa huru kufuatia kuchaguliwa kwa Louise Mushikiwabo kama mkuu wa Jumuiya ya nchi zinazoongea Kifaransa (Francophonie). Taarifa ya kukamatwa kwake ilitolewa na redio moja ya Rwanda, lakini hata hivyo haijathibitishwa na mamlaka.

Picha ya Kizito Mihigo inazozunguka kwenye mitandao ya kijamii. Kwenye picha hiyo, Mihigo anaonekana akiambatana na wanaume wengine wawili, wakiwa na begi chini ya miguu yao. Kulingana na shahidi mmoja aliyenukuliwa na vyombo vya habari nchini Rwanda, Kizito Mihigo alionekana Alhamisi wiki hii wilayani Nyaruguru akikaribia kwenye mpaka wa Burundi. Inasadikiwa kwamba wanakijiji waliripo polisi na kuweza kukamatwa.

Lakini polisi na Ofisi ya Uchunguzi ya Rwanda hawajathibitisha kukamatwa kwake. Ndugu zake wanaamini kwamba yuko kizuizini huko Nyaruguru, mkoa anakotoka. Lakini wanahoji ushahidi uliosambazwa na waandishi wa habari: "Nimeshangaa sana, hajawahi kuongea kuhusu kuondoka nchini Rwanda," amesema mmoja wa ndugu zake.

Hapo awali Kizito Mihigo alichukuliwa kama mtume wa maridhiano na mmoja wa waimbaji mashuhuri nchini Rwanda. Alikamatwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2014. Wakati huo alitoweka kwa siku kadhaa kabla ya mamlaka kuthibitisha kwamba anazuiliwa.

Kizito Mihigo ambaye ni mmoja wa watu walionusurika katika mauaji ya kimbari alikaa miaka minne kizuizini, akishutumiwa kuwa na uhusiano na upinzani wa kisiasa ulio na tawi la kijeshi uhamishoni. Mwishowe aliachiliwa mnamo mwezi Septemba 2018. Tangu wakati huo, hakukuwa na alinyang'anywa pasi ya kusafiri na kitambulisho na hakuweza tena kufanya shughuli zake za kimuziki.