http://s.rfi.fr/media/display/a191d85c-4430-11ea-9fd2-005056bfd1d9/w:1024/p:16x9/000_1oj3me_0.jpg
Jiji la Wuhan na mkoa wake, kitovu cha ugonjwa unaofahamika kama Corona,limetengwa tangu Januari 23, 2020.Hector RETAMAL / AFP

Ugonjwa wa Corona wazua hofu Afrika, mashirika kadhaa ya ndege yasitisha safari za China

by

Mashirika mawili ya ndege barani Afrika, Kenya Airways na Rwandan Air, yamechukua uamuzi wa kufuta safari zote kuelekea na kutoka China kwa muda usiojulikana. Virusi vya Corona vimeua watu zaidi ya 200 nchini China.

Kenya Airways imesema kuwa bado iko kwenye mazungumzo na wizara ya afya na wizara ya mambo ya nje kuhusu muda ambao ndege hizo zitaacha safari ya China.

Nchi mbali mbali zimeendelea na juhudi za kukabiliana na virusi hivyo ikiwa ni pamoja na China ambayo tayari imepoteza raia wake zaidi ya 200 ambao wamefariki dunia baada ya kuambukiwza virusi vya ugonjwa huo.

Nchini Uingereza watu wawili ndi wamegundulika kuwa na virusi vya Corona, kwa mujibu wa mkuu wa idara ya afya nchini humo.

Kufikia sasa watu 10,000 wameambukizwa virusi vya Corona nchini China.

Kwingineko duniani watu 18 wameambukiwza virusi vya ugonjwa hatari vya Corona. Marekani imethibitisha visa 6 vya watu walioambukizwa, huku Ujerumani ikithibitisha vifo vya watu watano.

Kufikia sasa raia 83 wa Uingereza na wengine 27 raia wa kigeni wanasifiri kurudi nchini Uingereza kutoka Wuhan , mji wa China ambao ndio chanzo cha mlipuko huo.

Siku ya Alhamisi wiki hii Shirika la afya duniani, WHO , lilitangaza kirusi cha Corona kuwa ni dharura ya kiafya duniani wakati kirusi hicho kikiendelea kusambaa kwa kasi. Kutoka Wuhan ambako ni kitovu cha ugonjwa wa homa ya Corona, msemaji wa Hospitali kuu ya mji Wang Jiliang anasema wanajizatiti kupambana na ugonjwa huo.