http://s.rfi.fr/media/display/c90f6708-2015-11ea-869f-005056a964fe/w:1024/p:16x9/000_1mn7e9_0.jpg
Askari wa vikosi vya Umoja wa Mataifa huko Beni, DRC, Novemba 26, 2019.ALBERT KAMBALE / AFP

DRC: Jeshi lajaribu kuwatuliza nyoyo raia baada ya mauaji mapya Beni

by

Waasi wa ADF wanaendelea kutekeleza mauaji dhidi ya raia katika mji wa Beni na viunga vyake, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Watu zaidi ya ishirini waliuawa jana Alhamisi huko Beni, siku moja baada ya mauaji mengine ya watu zaidi ya arobaini kutokea katika eneo hilo, usiku wa Jumanne kuamkia Jumatau wiki hii. Raia wameeleza masikitiko yao kutokana na hali hiyo wakiinyooshea kidolea cha lawama serikali ambayo imeshindwa kuwalindia usalama.

Watu zaidi ya 60 waliuawa ndani ya kipindi cha siku nne katika eneo la Beni, wengi kwa mapanga au shoka kulingana na mashirika ya kiraia. Wakaazi wa eneo hilo wamesema mauaji hayo yamekithiri, wengi wao wameanza kutoroka makaazi yao.Wameshutumu tena jumuiya ya kimataifa na serikali ya DRC kwa "kutowajali".

Raia wanaendelea kulengwa katika mashambulizi yanayotekelezwa na makundi mbalimbali ya silaha, Mashariki mwa DRC, hususan kundi la waasi kutoka Uganda la ADF.