http://s.rfi.fr/media/display/e1b6dcec-43fa-11ea-9318-005056bf87d6/w:1024/p:16x9/2020-01-28t172746z_1943104617_rc25pe9csrrf_rtrmadp_3_libya-security_0.jpg
Askari wa vikosi vya Marshal Khalifa Haftar aelekezea bunduki yake kwenye picha ya rais wa Uturuki Tayyip Erdogan iliyowekwa kwenye kifaru cha jeshi la Uturuki huko Tripoli, Januari 28, 2020.REUTERS/Esam Omran Al-Fetori

Umoja wa Afrika watoa muongozo kwa kuondokana na mgogoro wa Libya

by

Mkutano wa Kamati Kuu ya Umoja wa Afrika kuhusu Libya ulimalizika Alhamisi alasiri katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville. Kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli, Fayez el-Farraj, alihudhuria mkutano huo, huku mpinzani wake, Marshal Khaliha Haftar aliwakilishwa na wajumbe.

Mwisho wa mkutano huu, Kamati Kuu ya Umoja wa Afrika kuhusu Libya ilitoa muongoza unaotakiwa kufuata ili nchi hiyo iondokane na mgogoro unaoendelea kuikabili.

Kamati hiyo imependekeza kufanyike "mkutano wa maridhiano ya kitaifa".

Katika taarifa yake ya mwisho, Kamati Kuu ya Umoja wa Afrika kuhusu Libya imebaini kwamba "mgogoro wa Libya unanufaisha mitandao ya kigaidi na kuhatarisha usalama katika ukanda huo wa Kaskazini Magharibi mwa Afrika".

Mataifa wanachama hasa yameonyesha uungwaji wao mkono kwa hitimisho la mkutano uliofanyika jijini Berlin, nchini ujerumani, siku kumi zilizopita. Na wamekubaliana kuheshimu vikwazo vya silaha dhidi ya Libya .

Kamati hiyo imelaani nchi za kigeni kuingilia katika mgogoro unaoendelea nchini Libya na imetoa wito wa "kusitisha" mapigano mara moja.