http://scd.sw.rfi.fr/sites/kiswahili.filesrfi/dynimagecache/0/0/768/433/1024/578/sites/images.rfi.fr/files/aef_image/000_par8321490.jpg
Rais wa Tanzania John MagufuliAFP Photo/Daniel Hayduk

Tanzania yaadhimisha miaka 58 ya Uhuru

by

Leo ni siku ya mapumziko, wananchi wa taifa hilo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 58 ya uhuru kutoka kwa wakoloni wazungu Desemba 9, mwaka 1961.

Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika huku rais John Pombe Magufuli akifikisha miaka minne madarakani tangu achaguliwe ambapo katika kipindi chake kumeshuhudiwa mabadiliko ya uongozi, kufufuliwa kwa shirika la ndege la ATCL, kuboreshewa kwa sekta ya elimu, afya pamoja na ujenzi wa miundo mbinu inayiunganisha miji na nchi jirani.

Licha ya ukosolewaji wa Serikali yake na wanasiasa wa ndani na baadhi ya mataifa ya magharibi kuhusu masuala ya demokrasia, wananchi wengi hata hivyo wameendelea kuonesha kuwa na imani na Serikali katika kuleta mabadiliko.

Katika hatua nyingine barua ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA iliyokuwa ikisambaa jana kwenye mitandao ya kijamii, viongozi wake wamesema watashiriki sherehe za maadhimisho ya mwaka huu, ambapo itakuwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2015.

Hii ndio mara ya kwanza kwa maadhimisho haya kufanyika mjini Mwanza, eneo la kanda ya Ziwa.